Speaker of the National Assembly of Tanzania 2022 - |Deputy Speaker of the National Assembly 2015-2022 |16th Deputy Attorney General of Tanzania |Lawyer
Namuomba Mungu atujalie utajiri wa hekima, busara pamoja na kuwa na moyo mkunjufu kwa kuwa vyeo, mali na majigambo ni vitu vya kupita katika maisha, bali utu wema pamoja na hofu ya Mungu vitadumu milele na kuacha alama isiyofutika katika Maisha yetu ya Duniani.
Katika maisha tumebarikiwa uwezo wa kuona na kujua mambo yaliyo tokea jana na yanayotokea Leo hakuna ajuaye kesho yake itakuwaje, hivyo ishi na watu vizuri, kwa upendo na amani kwasababu hatujui kila mtu tunayekutana nae kesho atakuwa nani? au atakuwa sehemu gani?
Jokate my dear, nafurahi sana kila nikiangalia hatua zako za kuifanya Kisarawe, Pwani, Tanzania sehemu salama na njema kwa wote, hasa watoto wa kike. You rock! Am very proud of you. Go girl, greater heights! No limit, not even the sky
@jokatemwegelo
. Lots of love 💕
Leo kazi yetu Watanzania ni moja tu, kwenda uwanjani kwa wingi kuisapoti timu yetu ya
@simbasctanzania
, ili kuhakikisha inaibuka na ushindi. Do or Die.
#yeswecan
You fought a good fight Mr. President. You led Tanzania with integrity, honesty, commitment and hard work to fulfil your purpose in this world. We will miss you Baba. May the beautiful soul of HE BW Mkapa Rest in Eternal Peace. Amen.
Kila La heri
@simbasctanzania
, wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika nina imani mtapambana hadi tone la mwisho, YES WE CAN.
Watanzania tulipoungana kwa pamoja katika mashindano ya kuhifadhi QURAN TUKUFU Jijini Dar es Salaam. Hili ni jambo la kipekee sana kuwahi kutokea. Hii ni picha halisi ya amani na upendo.
Siku zote kumbuka kuwa unapolalamika kuwa umefeli katika maisha usisahau kuwa, kuna mwenzako ameshindwa kupata hata hiyo nafasi ya kufeli lakini wewe umefeli kwasababu umepata nafasi ya kujaribu ambayo kuna wengi wameikosa.
#TimizaMalengo2019
Jamii inahitaji kuwa na mtu ambaye anaweza kusimama na kufanya jambo kwa manufaa ya jamii nzima bali sio kwa manufaa yake, jamii inahitaji mtu anayeweza kusimama na kuyatetea maslahi ya wanyonge, mtu anayeweza kuhamasisha na kupigania maendeleo ya jamii.
As we join the Burundians to mourn the passing of HE Pierre Nkurunzinza, we are reminded that life is too short. Live a life that leaves a mark behind, however small. May his soul RIP.
#letlovelead
Una kila sababu ya kuishi kwa furaha na amani, usiumizwe sana na vikwazo au maneno ya watu bali uwe hodari na imara wakati wote ili uweze kutimiza malengo yako.
#tbt
#TuijengeTanzaniaYetu
Hapa Duniani unaweza ukatenda wema mpaka ukakosa nguvu za kwenda zako, hivyo kuwa makini na watu wanao kuzunguka maana moyo wa Mwanadamu ni kiza kinene huwezi kujua yupi ni mkweli na yupi ni muongo katika maisha yako.
Tanzania tumejaliwa kuwa na vivutio pamoja na mazingira mazuri na ya kipekee, nina kila sababu ya kujivunia kuwa Mtanzania kila nitembeapo naona uzuri wako wa asili na wa kuvutia. Daima nitakulinda na kukutunza Tanzania yangu. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.