Kuonekana Mwanaume si lazima ujiweke Mchafu Mchafu wazee, Jipendeni, Body spray imekushinda Bei Sugua hata Kipande cha Limao Kwapani, Chukua Brush Safisha Makucha hasa ya Miguu, Ukipiga Mswaki pia tumia hata Dakika Moja kusugua na Ulimi pia. JIPENDENI BASI MASELA
Kama Huna wewe HUNA tu, Ku Force Maisha ya Mitandaoni Kujifanya High Class na Maisha Safi sio Sawa Mwishoni mtu unakuja kuumbuka hivi hivi, Kilichokuja na Jahazi kinasema... DONT GO BROKE TRYING TO LOOK RICH, ACT YOUR WAGE.
S T A Y - I N - Y O U R - L A N E
Kuna Wana walikaa Juu ya Ghorofa wanasikilizia Risasi huku wanaongea "HIYO IMEPIGWA MBALI" kuna nyengine ikapigwa akasikika "HIYO SASA YA KARIBU" Yaani tunachambua hadi Sentimita za Mraba za Risasi... BONGO NYOSO 🙌
"Dogo Amerudi Hapa Ananiambia Baba Mwalimu Ameniambia Unisaidie Kujiandaa na Debate...Nikamuuliza Topic gani, Akasema e
Education is Better Than Money. Nikamuuliza uko upande Upi, Akasema, Yeye ni Opposer. Nikamwambia You are on The right Side, Kula Ushibe Nikupe Madini 😄😄😄"
Kuwa Single Mother haikufanyi uwe Baba au ujipe vyeo vya kuwa Baba. Msinyime Watoto haki zao za Msingi na Kuwajua Baba zao. Mtoto hajakosana na baba ake ila wewe ndio uliekosana na Mwanaume wako.
Pierre Baba wa Watu Anakula zake Maisha hana Tabu na mtu Aiseee, Pierre hakuomba kuwa maarufu.... watu walimkuta anakunywa zake bia wakamrekodi wakasambaza clips and the rest is history, Kosa lake ni lipi? Mungu ameshapanga kila mtu jinsi atakavyopata mkate wake wa kila siku. 🙏
Mungu akikupa Neema ya Kupata Mtoto, Mjali Sana, Mpende Sana, Mpe Malezi Zaidi ya Uliyopewa, Mpe Elimu Zaidi ya uliyopewa, Mpe Attention, na Kikubwa Zaidi Mpe Mafundisho ya KUMUOGOPA MUNGU.
Heri ya sikukuu ya Eid Al Fitr kwa waislamu wote Tanzania!
👉Allah apokee funga zenu na swala zenu.
👉Awajaaalie amani na upendo mioyoni mwenu na haki katika siku zenu hapa duniani na awaandalie akhera njema! 🙏
Watanzania Ni Dharau au elimu bado ndogo ya hili gonjwa? KARIAKOO, MASOKONI, MANZESE watu hawana habari kabisa yaani hadi ukifika kule unaanza kujistukia peke yako ndio muoga.
Mpira ni Biashara, Mchezaji, Kocha au hata Tajiri anaweza kuhama Timu basi Siwezi Kumlaumu HAJI MANARA kwa kuhamia sehemu yenye Maslahi na Yeye, Ni Biashara pia Kama Kaondoka Messi pale Barcelona. Kutoka Kulipwa Laki 7 hadi mamilioni hata mimi ningehama kwa timu ya mama angu.