Mhe. Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amefanya kikao na LATRA, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Mmiliki wa kampuni ya mabasi Kilimanjaro Express ili kujadili kufungiwa kwa huduma za Usafiri kwa kampuni hiyo.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani imefungia Leseni za Magari 36 pamoja na madereva 10 kwa makosa mbalimbali ikiwemo mwendokasi hatarishi na kuingilia Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS)
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imefanya ukaguzi wa kushtukiza kwa Mabasi ya masafa marefu ili kutathimini hali ya Usafiri nchini, Januari 6, 2024.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imerudisha ratiba na leseni za mabasi 38 ya kampuni ya New Force kuanzia tarehe 11 Septemba, 2023. Mabasi hayo yataanza safari zake muda wa 9.00 usiku na saa 11.00 alfajiri.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imedhamini zawadi ya mwanafunzi bora wa shahada ya Usimamizi wa Vifaa na Usafiri kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeendelea na ukaguzi wa Masharti ya Leseni kwa Mabasi ya mjini (Daladala) Mkoani Dar es Salaam ambao hufanyika kila siku.
@TBoundBuses
@WizarayaUJnaUC
Kanuni za LATRA zinaelekeza mabadiliko (modification) yoyote inayofanywa kwenye bodi za magari ya abiria kupata kibali cha TBS na kampuni iliyounda gari husika.
LATRA hutoa Leseni za Usafirishaji baada ya kupata taarifa safi ya ukaguzi kutoka Jeshi la Polisi (VIR)
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeendesha mafunzo ya usalama barabarani kwa maafisa wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kuchukua hatua dhidi ya dereva wa Kampuni ya Super Feo aliyebainika kuendesha basi mwendo hatarishi bila kuzingatia Sheria.
CPA Habibu J. Suluo, Mkurugenzi Mkuu LATRA akiambatana na Wakuu wa taasisi na viongozi mbalimbali wa serikali kukabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi bilioni mbili kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
@TBoundBuses
Habari, wasafirishaji wamepewa ratiba tofauti ili kuepusha Hali ya kushindana wakiwa barabarani, hii itasaidia kupunguza hatari ya kupata ajali kutokana na mwendokasi
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Arusha imewatembelea wadau wa Usafirishaji wakiwemo madereva na makondakta wa Mabasi ya mjini (Daladala) mahali pa kazi na kutoa Elimu ya utekelezaji wa Masharti ya leseni, Aprili 23, 2024.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imerudisha ratiba ya mabasi 9 yaendayo mikoani mali ya Kampuni ya Ally's Star na Katarama Luxury,
Ratiba zimerudishwa baada ya mabasi hayo kuyafungiwa kutokana na makosa ya ukiukaji wa masharti ya Leseni.
@PhysicsJ7
@TBoundBuses
@tanroas
@SouthernBuses
Habari, tiketi halali inapaswa kujumuisha taarifa za nauli iliyolipwa pamoja na muda wa safari, Ni wajibu pia wa abiria kuhakikisha taarifa zote za msingi zipo kwenye tiketi yake, pia kwa changamoto yeyote unaweza kutoa taarifa moja kwa moja kwa Mamlaka kupitia namba 0800110019
Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezindua rasmi Kanzi Data (Data Base) ya Chama cha Wamiliki wa Maroli Tanzania (TATOA) ambayo itatumika kuwasajili na kutunza taarifa rasmi za madereva wa maroli.
Katika mkutano huo Mhe. Chalamila amemtaka Mmiliki wa kampuni hiyo kutimiza matakwa ya LATRA kikamilifu kama ilivyoelekezwa kwenye barua ya kufungiwa huduma ili kuruhusiwa kutoa huduma.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeendesha Mkutano na wadau wa Usafiri Ardhini ili kufanya tathmini ya Mpango Mkakati wa Mamlaka wa 2020/21 Hadi 2024/25.
Wadau mbalimbali watembelea banda la LATRA lililopo kwenye maonesho ya 16 ya wadau wa Sekta ya Uchukuzi yanayofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) - Arusha kuanzia Disemba 5 - 8, 2023.
Wadau mbalimbali watembelea banda la LATRA lililopo kwenye maonesho ya 16 ya wadau wa Sekta ya Uchukuzi yanayofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) - Arusha kuanzia Disemba 5 - 8, 2023.
Vigezo vilivyowekwa ili kuruhusiwa kutoa huduma ni pamoja na Kutumia Mfumo wa Tiketi Mtandao ulioidhinishwa na LATRA, kuweka nauli isiyozidi viwango vilivyowekwa na Mamlaka, na Kutuma maombi kwa Mamlaka yakionesha namna watakavyodhibiti makosa haya yasijirudie.
CPA Habibu Suluo, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA anatarajia kufanya Mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari nchini Oktoba 19, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Golden Jubilee, Dar es Salaam
Mamlaka Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea tuzo ya shukrani kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kudhamini maadhimisho ya Miaka 20 ya TCAA
LATRA yakutana na wamiliki wa mabasi ya mjini (Daladala) ili kuboresha huduma za usafiri jijini Arusha.
Aidha, LATRA Kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha imetangaza maegesho rasmi ambayo pikipiki za magurudumu matatu (Bajaji) zinapaswa kuegeshwa.
🎥:
@millardayo
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani waendelea kufanya tathmini ya hali ya usafiri wa vyombo vya moto kibiashara katika kipindi cha Sikukuu za mwisho wa mwaka nchini kote.
Mhe. Atupele Fred Mwakibete, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) ametembelea banda la LATRA na kuipongeza Mamlaka hiyo kwa kazi nzuri ya udhibiti wa huduma za usafiri wa abiria na mizigo kwa kutumia mifumo ya TEHAMA, .
Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA, pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya LATRA wametembelea baadhi ya maeneo yanayotoa huduma za usafiri wa mabasi mkoani Dodoma, ili kujifunza na kupokea changamoto zinazowakabili wadau ili kuzitafutia ufumbuzi 26 Octoba, 2023.
CPA Habibu Suluo, Mkurugenzi Mkuu LATRA leo Disemba 5, 2023 amewasilisha mada katika Mkutano wa 16 wa Wadau wa Sekta ya Uchukuzi unaofanyika Mkoani Arusha Disemba 5 - 8, 2023 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa - Arusha (AICC).
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inafanya ukaguzi katika vituo mbalimbali vya mabasi ya mjini (Daladala) ili kukagua utekelezaji wa masharti ya Leseni za Usafirishaji
Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi amezindua Bodi ya Pili ya Wakurugenzi ya LATRA leo Jumanne Julai 11, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano kwenye Ofisi ya LATRA Mkoa wa Dar es Salaam.
SUMATRA jana ilitunukiwa Tuzo ya NBAA Mshindi wa Kwanza kwa Kuandaa Taarifa za Fedha kwa Kiwango cha Kimataifa katika kundi la Mamlaka za Udhibiti mwaka 2017
Mkurugenzi Mkuu Gilliard Ngewe amekabidhiwa tuzo hiyo na Mgeni Rasmi Naibu Waziri-Fedha na Mipango Mhe. Dr. Ashatu Kijaji
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) yainuka kidedea katika kipengele cha Banda Bora la Wadhibiti kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Tanzania -SABASABA
@TBoundBuses
@j_shauritanga
Nadhani hata Wewe unaweza kuona kuna tatizo endapo gari lilioanza safari saa 10 alfajiri likamaliza safari muda ambao gari lilioanza safari saa 9 lilitakiwa kumaliza safari
Mhe. Edward Jonas Mpogolo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala amewatunuku vyeti vya uthibitisho madereva 1518 waliofanya mtihani na kuthibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini na kufanya jumla ya madereva 2517 waliothibitishwa.
Usikose kipindi cha SUMATRA TBC1 leo Alhamis saa moja na nusu jioni. Utaufahamu vzr mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi (VTS) na yanayojiri sasa ktk mfumo huo