Benard Morrison atakosekana mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar kwa sababu za kifamilia.
Lakini katika picha anaonekana akizindua Taasis yake ya Benard Morrison nchini 🇬🇭Ghana.
#KupangaKuchagua
#UsiaminiVicheko
Mudathir anacheza namba 10
Aziz Ki anaanzia benchi
Hana Feitoto
He is Profesa
NB: Njia pekee ya kuwazuia Yanga Nabi apewe TIMU YA TAIFA au Aondoke nchini.
Baada ya mchezo hapo jana , Rais wa 🇫🇷 Ufaransa Emanuel Macron alitembelea vyumba vya kubadilishia nguo vya tumu ya Taifa ya 🇲🇦Morocco na kumuambia Sofyan Amrabat mbele ya wenzake kuwa"wewe ndie kiungo bora mkabaji wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022...."
#EKsports
|| Klabu ya Simba imeuchagua uwanja wa New Amaan Complex wa visiwani Zanzibar kuutumia kwenye michezo yake ya kimataifa na ya ndani [Ligi ya mabingwa Afrika, FA na Ligi Kuu.
MAENDELEO NI MCHAKATO...
🇹🇿 Simba SC vs 🇲🇦Wydad (Wydad Mabingwa Ligi ya Mabingwa × 3)
🇹🇿Simba SC vs 🇿🇦Mamelodi ( Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika ×1 ).
🇹🇿Simba SC vs 🇹🇳 Esperance (Esperance ni Mabingwa ×4 Ligi ya Mabingwa Afrika).
Maisha yanaenda Kasi sana.......
" Mtanzania pekee kuwepo katika kikosi cha WIKI cha Ligi ya Mabingwa Afrika Raundi ya 5 kutoka kikosi cha Simba SC lakini bahati mbaya hayupo kuwakabili 🇺🇬Uganda ........"
Mdau DM
#UsiaminiVicheko
Kilipotoka Kikosi cha Yanga SC na wengi kuona Jonas Mkude ameanza na Aucho hayupo maswali yalikuwa mengi sana.Binafsi naamini Mpango kazi wa mwalimu unaanzia mazoezini...
Mchezaji mkubwa katika mechi kubwa.Uzoefu na nidhamu ya mchezo kwa Jonas Mkude.
Maana YA UDUGU UMALA ndio hii sasa....
Nabi na Kaze kutoka 🇹🇿Yanga SC kama Kocha Mkuu(Nabi) na msaidizi wake(Kaze) mpaka 🇿🇦Kaizer Chiefs kama Kocha Mkuu na msaidizi wake.
"Mchambuzi,mbona Dejan Georgijevic alivunja mkataba kupitia instagram na klabu ikamalizana naye kiroho safi.Lakini huyu mwingine mpaka kwa PILATO....?...."
TARATIBU ZIFUATWE
Pep aliijenga 🇪🇦Barcelona akaondoka
Zidane aliijenga 🇪🇦Real Madrid akasepa
Carlo Ancelloti aliijenga 🇮🇹 Ac Milan akasepa
Sir Alex Ferguson aliijenga 🏴Manchester United naye akasepa
Profesa ...........
JONAS MKUDE
Miongoni mwa wachezaji wachache nchi hii kuitumikia klabu moja pekee katika maisha yake ya Soka na bado anaendelea kuitumikia klabu hiyo.
Legend wa Simba SC
....Sijui tumeishiwa vya kujadili. Sijui huwa tunawaza nini. Sijui nani aliileta hii stori ya Bus la Simba kurudi kinyumenyume. Soka letu lina mengi ya kuyajadili kuliko hili Bus la Simba. Nchi haina kocha wa timu ya Taifa. Nini tufanye?
#EKsports
|| Hii Yanga ni bora zaidi ya msimu uliopita, inakupa burudani na magoli pia, hii kampeni ya goli tano itakuja kutufanya timu zingine zisiingize timu uwanjani😃.
FT: YANGA 5-0 JKT TANZANIA.
#EKsports
|| Nyota wa klabu ya Simba Pape Ousmane Sakho amemtakia kila la Heti nyota mpya wa kikosi hicho Luis Jose Miquissone ambaye ataivaa jezi namba 10 msimu ujao, ikumbukwe pia Sakho alikua akitumia namba hiyo akiwa Simba.
#EKsports
|| Baada ya mazungumzo marefu baina ya upande wa Yanga na Fiston Mayele hatimae mambo yameeleweka na atatimkia Pyramids ya Misri baada ya mchezaji mwenyewe kuomba kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.
#EKsports
|| Leo klabu ya Simba imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kipanga ya Zanzibar na kumalizika kwa matokeo ya Ushindi wa goli 3-0.
Magoli ya Simba yamefungwa na Aubin Kramo, Moses Phiri na Luis Miquissone
#EKsports
|| Msimu huu katika ligi ya mabingwa klabu ya Simba itaanzia hatua ya pili kuelekea makundi sawa na vilabu vya Wydad AC, Al Ahly, Esperance, Mamelod Sundowns, Petro de Luanda, TP Mazembe, Enyimba, CR Belouzdad na Pyramid fc.
"Si nchi zote zinawawakilishi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23.
Kama 🇹🇿Tanzania tuna kila sababu ya kusema ni hatua kubwa sana kama NCHI katika maendeleo ya SOKA ......"
Jean Charles Ahoua sio mchezaji mbaya hata kidogo ila kwa Awesu Awesu kocha Fadlu anakuwa machaguo mengi ya eneo la ushambuliaji kutokea katika kiungo.
Awesu Awesu top 🇹🇿Tanzanian talent
"Wamezoea maisha haya ...
Wanaitangaza nchi kila sehemu ikija kutoka makundi kwenda Robo fainali
Hawana presha kabisaaaa
Fahari ya nchi michuano ya kimataifa......"
Mdau
#EKsports
|| Kwa mujibu wa shirika la tafiti na habari Duniani la IFFHS limeitaja klabu ya Yanga kama klabu namba tatu (3) Barani Afrika ikiwa nyuma ya Al Ahly na Wydad Casablanca.
Hizi ni takwimu za kuanzia mwezi wa tisa (9) mwaka Jana hadi mwezi wa nane (8) mwaka huu.
Hakuna timu imchukue hata kwa mkopo acheze Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho ...
Ubora wake na uwezo wake unatosha sana kumfanya acheze makundi Michuano ya Afrika ngazi ya klabu msimu huu.
#KupangaNiKuchagua
Maisha yanaenda kasi sana Duniani
Kocha Fadlu Davids akiwa na makocha wenzake Rulani Mokoena na Micho.
FT: Azam FC 0-2 Simba SC
Simba SC ya Fadlu Davids Michezo 3 ya Ligi
✅️Kushinda 3
✅️Magoli 9
✅️Clean sheet 3
#EKsports
|| Young Africans imekamilisha usajili wa mkopo wa mshambuliaji wa Kaizer Chiefs Ranga Chivaviro usajili ambao utatambulishwa kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi January.
Edwin Balua nje ya kikosi cha 🇹🇿Taifa Stars...
Sasa hivi Timu ya Taifa kuna wachezaji kutoka Fountain Gate, KMC , Pamba ,Singida Black Stars nk
Maisha yanaenda kasi sana
Baada ya msimu wa mateso kwenye klabu ya Manchester United kumalizika, nyota wa klabu hiyo Sofyan Amrabat amekuja kufurahia likizo yake kwenye mbuga ya
@mikumi_nationalpark
Tanzania imekuwa sehemu salama sana kwa wachezaji mbalimbali Duniani kujivinjari.
#EKsports
|| Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema sababu ya kuipamba zaidi jezi namba sita ni kwasababu za kibiashara zaidi, pia jezi namba sita ilikuwa ni kwaajili ya burudani kwa mashabiki.
Kamwe amesema Yanga imeingiza pesa nyingi katika utambulisho.
#EKsports
|| Kwa mujibu wa shirikisho la soka nchini Sudan limethitisha mchezo kati ya El Merreikh dhidi ya Yanga SC utachezwa nchini Morocco badala ya Rwanda ambapo waliitumia kwenye mchezo wa hatua ya awali.
Mtibwa walishaamua kuchukua njia yao ya kupata wachezaji.Shida ni moja tu wanajiendesha kimazoea na hawataki kushindana kupata nafasi ya kucheza Michuano ya Kimataifa pamoja na rasilimali walizonazo.
Maisha ni HATUAA....
Mwaka 2020 Arsenal ilishinda Kombe la FA ikiwa na kikosi hicho hapo katika picha.Leo wanaongoza LIGI pasipokuwa na mchezaji hata mmoja kati ya wale waliochukua Kombe la FA.
AMINI MCHAKATO....
Klabu ya 🇿🇦Mamelodi Sundowns bado wana nia ya kumsajili kiungo wa klabu ya Azam na Timu ya Taifa ya 🇹🇿 Tanzania Feisal Salum 'Feitoto' kwa ada ya USD 1.8M (Tshs 5.4B) .....
Novatus Dismas aka Alessandro Bastoni
Sitoshangaa baadae nikimuona Ufaransa au Ujerumani au Hispania.Ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.
✅Beki wa kushoto
✅Beki wa Kati
✅Kiungo
Kwa umri wake ana nafasi ya kukua zaidi.
✔️Msemaji wao ni mmoja
✔️Timu haina Kombe la Ligi wa Kombe la TFF
✔️Wachezaji wao wachache wanajulikana
✔️Kocha mpya na benchi jipya la ufundi
✔️Wamejaza Tamasha lao.....
#EKsports
|| Klabu ya Mamelod Sundowns inataraji kutua nchini Tanzania wakati wowote wakitokea nchini Afrika Kusini kwaajili ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Bumamuru ya Burundi utakaopigwa ijumaa hii.
Thamani ya Kikosi cha 🇩🇿MC Alger ni Euro 15 Milioni (Tsh 44.8 Bilioni).
🇩🇿MC Alger wapo Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi A
1.🇨🇩TP Mazembe
2.🇸🇩Al Hilal
3.🇹🇿Yanga SC
4.🇩🇿MC Alger
"Kama nikipewa kuiongoza ile timu ya Azam naweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu mara Nne (4) mfululizo, kwasababu wana miundombinu yote ya kuwafanya wabebe ubingwa."
Julio
- Kocha wa KMC