Askofu Emmaus B Mwamakula Profile Banner
Askofu Emmaus B Mwamakula Profile
Askofu Emmaus B Mwamakula

@EmmausAskofu

52,912
Followers
73
Following
132
Media
528
Statuses

Bishop, Author, Theologian, Missiologist, Activist, Poet, Lecturer, Sociologist, Missionary, Political Analyst, Social Analyst and Counselor.

Joined April 2021
Don't wanna be here? Send us removal request.
Pinned Tweet
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kuna watu wametengeneza akaunti feki ya twita kwa jina langu! Hii hapa siyo Akaunti yangu. Epuka utapeli huu!
Tweet media one
20
42
204
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Tunatangaza maombi ya siku 7 mfululizo kwa ajili ya kumuombea Freeman Mbowe kuanzia leo Jumatatu 26 Julai 2021. Watu wakusanyike katika vikundi majumbani au watumie muda wa maombi kila siku kabla ya kulala wakilitaja jina la Mbowe mbele za Mungu. Neno la kusimamia ni Zaburi 20:7
Tweet media one
144
431
3K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Jeshi la Polisi Mwanza walinifuata hotelini mimi na Prof. Lwaitama tulioalikwa kutoa mada katika Kongamano la Katiba lililoandaliwa na BAVICHA. Walitukamata na kutuweka kizuizini kwa zaidi ya saa 30 na wafuasi na viongozi wa CHADEMA. Tunawashukuru kwa kutupazia sauti. Tumeachiwa!
Tweet media one
118
228
3K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini! Hotuba yake imebeba mawazo mbadala katika nchi. Viongozi wa Serikali hawapaswi kuijibu kwa mipasho na kebehi. Bali wanapaswa kuketi na kuitafakari kwa umakini kwani imebeba hisia na maumivu ya Watanzania walio wengi!
75
186
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kigogo hana tofauti na Kalagesye! Kwa msiomjua Kalagesye, tafuteni kitabu cha Kiingereza cha Darasa la 6 cha miaka ya 1970 na 1980. Tofauti ya Kigogo na Kalagesye ni moja tu nayo ni kuwa Kigogo anaonekana kuwa ni taasisi! Nani kagudanganya kuwa mitandao ya kijamii ilianza juzi?
Tweet media one
37
136
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Tumetumia Facebook kutangaza maandamano ya nchi nzima kushinikiza Serikali kuacha kutumia Jeshi la Polisi kuzuia watu kutoa maoni kuhusu Katiba wanayotaka, kuzuia mikutano ya kisiasa, kuachia mahabusu wa kisiasa, nk. Sisi Askofu na viongozi wengine wa dini tutaongoza maandamano!
Tweet media one
129
284
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
Waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania kesho watasomewa waraka wa Maaskofu wa TEC wa kuupinga Mkataba wa Bandari! Kama Chongolo, RC Chalamila na IGP Wambura ni Wakatoliki watasomewa pia! Hayo sasa ni maandamano makubwa ya kupinga Mkataba wa Bandari yasiyohitaji kibari cha Polisi!
108
300
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Sisi Askofu Mwamakula, tunapenda kuwajulisha kuwa tunajiandaa kuongea na Watanzania na dunia kwa ujumla kupitia Vyombo vya Habari. Tutazungumza kuhusu jinsi mambo yanavyokwenda nchini. Maandalizi yakikamilika, tutatangaza tarehe na mahali tutakapofanyia Press. Ezekieli 33:1-20
Tweet media one
59
196
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Leo nilitoa mada Segerea katika Kongomano la Katiba la BAVICHA. Mada yangu ilihusu "Mtazamo wa Kidini Kuhusu Mabadiliko ya Katiba". Ushahidi wa niliyoongea umenaswa kwa vinasa sauti. Wanaosambaza maandishi kuwa niliongelea mahusiano ya jinsia moja wamepagawa na mapepo ya uwongo.
46
157
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
13 days
Tumearifiwa kuwa Charles Chaula alitekwa jana kijijini Ntokela Kata ya Ndato, Rungwe, Mbeya. Waliomteka walifika na gari nyeusi wakampakia. Kama atadhurika, basi waliomfungulia mashtaka hapo awali ndio watakaobeba lawama. Tunataka kujua yuko wapi na amekamatwa kwa kosa gani!
Tweet media one
69
402
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa aliniuliza: "Askofu, kwa nini umekubali kuwa Mshauri wa Tundu Lissu"? Nikamjibu: "Kwa nini nikatae kuwa Askofu Mshauri wa Tundu Lissu"? Alinyamaza kimya! Kwa nini watu wengine hawapendi kuona viongozi wa upinzani wanakuwa karibu na Maaskofu?
42
114
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kesho nitakuwa Ukumbi wa Boma Hotel uliopo Nyakato National mjini Mwanza kuanzia saa 4:00 asubuhi ambapo nitakuwa natoa mada kuhusu Katiba Mpya. Nimealikwa na BAVICHA. Karibu unisikilize ukumbini au live kupitia mitandao ya kijamii.
Tweet media one
48
122
2K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Watu wasio wa kawaida wenye sifa za UFO - Unidentified Flying Objects wapo karibu na Hoteli aliyofikia Askofu Mwamakula eneo la Nyakato, Mwanza. Nyendo zao zilijifunua zaidi kuanzia saa 12 jioni. Kama wana agenda yenye hila dhidi ya Askofu, Mungu atazifanya njia zao kuwa utelezi!
Tweet media one
57
186
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Tumeelezwa kuwa Freeman Mbowe, Dr. Lwaitama, John Pambalu , John Heche na watu wengine 7 wamekamatwa na Jeshi la Polisi mjini Mwanza baada ya kuizingira hoteli. Wengine wote wapo Polisi lakini Mbowe haijulikani aliko. Sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito wa kuachiliwa kwa watu hao.
Tweet media one
61
228
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Rais Samia asipoingilia kati kuamrisha Askari waache kupiga na kuua Wamasai kwa risasi kule Umasaini, sisi Askofu Mwamakula tutatoa wito wa kuitishwa Mkutano wa Wamasai wote waishio Dar es Salaam, Pwani na Morogoro na sisi tutakuwa sehemu ya maandamano hayo. Sambaza ujumbe huu!
103
310
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Tumesikia CHADEMA, ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi na CUF havishiriki Kikao cha Vyama vya Siasa kilichoitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi. Tungeshangaa kama vyama vikuu vya upinzani vinavyotakiwa kutoa muelekeo wa kidemokrasia nchini vingeshiriki kuvunja Katiba!
Tweet media one
58
200
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Masaa 3 kabla Mbowe hajakamatwa tuliketi meza moja kwa chakula kilichoandaliwa kwa heshima yetu. Nilimwambia ale na anywe kwani baada ya hapo jambo zito lilikuwa mbele yake. Leo ni siku ya 29 tangu akamatwe na kuwekwa ndani. Sikuwa nakula chakula na gaidi, bali na mwanaharakati!
Tweet media one
52
182
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Sheria za Kimataifa hazizuii kuandamana kwenda Ubalozi kutoa hisia. Kama BAWACHA mlifanikiwa kuingia Ubalozi wa Marekani kushinikiza Mbowe aachiwe, hamjavunja Sheria ye yote. Kukamatwa kwako Neema Mwakipesile ni chokochoko za Katiba Mpya! Tunataka uachiwe pasipo masharti ye yote
Tweet media one
45
191
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Msihangaike na matunda, hangaikeni na mti wa matunda. Wabunge 19 ni matunda ya Uchaguzi Mkuu ulioharibiwa! Msiogope kuwasema walioharibu Uchaguzi na kuleta taharuki CHADEMA. Matunda yanaweza kuoza lakini mti utaendelea kuwepo. Ushughulikieni huo mti muone kama matunda yatakuwepo!
52
128
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Jana nilifika Mahakamani kusikiliza Kesi ya Mbowe na wenzake, niliona mengi. Njiani nilikuwa na watu 3 waliokuwepo. Mmoja akanieleza jambo, nikashauri amjulishe Wakili! Baada ya tafakuri asubuhi nikaandika Litania Maalum ya kuombea Kesi hiyo! Mungu amejidhihirisha! Usiache kuomba
Tweet media one
35
126
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
Tumepokea tahadhari kuwa sisi Askofu Mwamakula pia hatuko salama sana. Sisi hatuogopi na hatutakimbia. Sehemu ya wito wetu ni kuwa sauti ya wengine hata ikibidi kuhatarisha maisha yetu. Tegemeeni lo lote kutoka kwetu isipokuwa kukata tamaa, kuogopa au kusaliti utetezi wa haki.
52
280
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Risasi 16 zilizoingia mwilini mwa Lissu zilimjenga sana kisiasa. Kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe inamuinua zaidi Mbowe na kumfanya shujaa! Lissu na Mbowe ni phenomena mpya Tanzania na Afrika! Hawa watu kwa pamoja wataushangaza ulimwengu! Tunzeni ujumbe huu wa Askofu Mwamakula!
57
161
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Mbunge wa Viti Maalum anasema Bungeni kuwa aliondolewa Uanachama na Chama chake! Naibu Spika anamtaka afute kauli kwa kuwa Ofisi ya Spika haina taarifa hiyo. Wafuasi wa CHADEMA wanamwaga mitandaoni nakala za barua ya Chama chao kwenda kwa Spika! Rais Samia atateswa na mambo haya!
45
93
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Msimchukie wala msimtukane Dkt. Mwigulu Nchemba kwa sababu ya Tozo! Mkosoeni kwa hoja. Kumtusi na kumchukia ni udikiteta pia na ni kuonyesha kuwa mngekuwa na madaraka mngempoteza kama utawala ule ulivyokuwa unapoteza wenye mawazo tofauti! Kuweni wakomavu kwa kuwavumilia wengine!
218
106
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
10 months
Msaidizi maalum wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania, Mhe. Tundu Lissu; ameshambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam jana, 30 Oktoba 2023 majira ya saa 2 usiku. Hizi ni dalili za giza la kisiasa kuanza kutanda tena!
Tweet media one
193
211
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Mheshimiwa Mbowe atuma ujumbe mzito kwa Watanzania. Asema viongozi wengi nchini ni wasaka fursa. Asema kuwa ipo ambayo umaskini na ujinga vitatokomezwa. Awashukuru wote kwa kumuombea!
Tweet media one
37
148
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
8 Agosti 2021: Askofu Mwamakula na Askofu Mwamalanga, wametembelea mahabusu wa kisiasa. Wamemuona Mbowe (Ukonga), Gelvas Lyenda na wenzake 11 (Mburahati) na Catherine Ruge na wenzake 29 (Central Police). Afya ya Mbowe iko vizuri na amewaomba Watanzania kuungana kudai Katiba Mpya.
Tweet media one
35
161
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Tawala nyingi zilianguka baada ya kuanza kutesa na kuua na kuumiza watu wake. Dalili za mwanzo za kuanguka kwa utawala wowote duniani ni utawala husika kuanza kutesa, kuumiza na kuua watu walio na mawazo tofauti na watawala!
43
185
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
BALOZI DKT. SLAA AKAMATWA NA POLISI! Ndugu Watanzania! Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amekamtwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake muda huu. Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate! Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Tweet media one
77
232
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Rais Samia si mtawala wa kijeshi! Kitendo cha usalama kufuatilia kila anayejadili kupinga tozo kwenye makundi ya Wasapu ni aibu kubwa. Mnazuia watumishi wa umma kutoa maoni kuhusu tozo zinazowaathiri? Mnataka mashetani ndio watoe maoni? Mrudisheni Jonas Afumusye Mwangunga kazini!
45
147
1K
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilituhumiwa kuvuruga CUF. Baadaye ikatuhumiwa kuhusika na utata wa Wabunge wanawake 19 kutaka kuvuruga CHADEMA. Sasa inatuhumiwa kuvuruga NCCR Mageuzi kwa kutumika kuleta mgogoro ndani ya NCCR. Nani ataikemea Ofisi hiyo kama sote tutanyamaza?
60
137
999
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Lazaro Nyalandu! Nimewasihi CHADEMA wasikushambulie! Lakini wana hasira sana na wewe kwa kauli ulizotoa! Wana sababu kama unawasimanga! Mimi ni shahidi jinsi walivyokupokea kwa upendo na kukuamini. Wewe sio mshenzi, bali ni muungwana. Twiti yako moja ya kuomba msamaha itatosha!
57
80
975
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Wawekezaji na Demokrasia ni sawa na mtoto na mbeleko! Ikikatika mbeleko, mtoto huanguka! Ukiminya Demokrasia, wawekezaji hukimbia! Huwezi kumnyima pumzi mama mjamzito ukategemea kuwa mtoto aliye tumboni akaendelea kuishi! Miujiza ya aina hiyo bado haijatendeka katika uso wa dunia
34
150
978
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Mwambieni Fatma Karume! Vyama vya Wafanyakazi vya Tanzania vimepoteza uhuru wao kwa Serikali. Havina uwezo wa kujadili (negotiations) kwa niaba ya wanachama wao. Hivyo, Wafanyakazi wataendelea kutegemea fadhila ya Serikali ambayo kimsingi hutegemea na Rais ameamkaje mwaka huo!
32
74
945
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Spika Ndugai anaiona barua ya Katibu Mkuu wa CHADEMA kama kipeperushi kwa kuwa haina viambatanisho vyenye miniti na Katiba ya CHADEMA. Katiba ya nchi ndivyo inavyotaka? Hivi barua yenye majina ya Wabunge 19 ilikwenda na viambatanisho? Tafuteni muafaka msijifiche kwenye hoja mfu!
32
93
945
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
14 days
Taarifa kutoka Dodoma ni kuwa gari za STL ni nyingi kama utitiri katika Uchaguzi wa TLS. Ina maana mawakili wa Serikali wamejitokeza kwa wingi kupiga kura mwaka huu kuliko mwaka mwingine wowote katika historia ya Uchaguzi wa TLS. Tunaamini wapiga kura wameona pia ujumbe wa Askofu
25
122
983
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Nasisitiza kuwa Akaunti ya Twitter inayotumia username ya @EmmausMwamakula siyo ya Askofu Mwamakula. Watu waovu wameitengeneza kuhadaa umma. Huko nyuma waliitumia kumshambulia Fatma Karume! Sasa wanaitumia kumpongeza Zitto Kabwe kuhusu kauli aliyoisema mbele ya Rais juu ya Mbowe!
58
143
872
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
As religious leaders, we have warned the Police Force in Tanzania not to use excessive force against civilians who will be attending the Kisutu Residency Court to witness the proceedings of the case facing the opposition leader, Freeman Mbowe who is facing charges on terrorism.
Tweet media one
22
151
844
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
January Makamba ameongea mambo muhimu sana ya kuponya Taifa. Ametumia Bunge kuwaambia Watanzania kuhusu umuhimu wa kuheshimu uhuru wa kutoa maoni. Kwa mtazamo wangu, watu aina ya January ndio wanaoweza kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kuliunganisha Taifa katika wakati kama huu!
37
92
843
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Machinga wameanza kuwasha moto wa Katiba Mpya! Moto huu utaenea kila kona ya nchi. Ni ujumbe kwa watawala, sauti ya watu haiwezi kuzimishwa kwa mtu wa bunduki! Umma ukiamua hupumua na hakuna atakayeweza kuzuia pumzi yao!
Tweet media one
42
135
844
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Mheshimiwa Freeman Mbowe! Nakupa pole kwa msiba wa kaka yako. Hata katika majonzi mazito umeonyesha kuwajali Watanzania! Umeutangazia umma kuwa ndugu yako amekufa kwa Covid 19 na hivyo umewaasa kuendelea kuchukua tahadhari. Mungu awafariji mnapopita katika kipindi hiki kigumu!
11
77
840
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Waziri wa Kilimo Zanzibar ameamrisha kutaifisha tenga 30 za ndizi za Veronica Mwanjala, mjane wa watoto 2 kutoka Dar es Salaam na kumlipisha faini ya Sh. 50,000 akisema soko la ndani la Zanzibar halihitaji ndizi za Bara. Video inaonesha maofisa wa wizara wakipekua ndizi hizo.
298
317
846
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kama Taasisi za Dini zimefungwa midomo, kuondoa utaratibu wa usajili wa kudumu ili ziombe upya usajili kila baada ya miaka mitano ni kuzichimbia kaburi. Ukifanikiwa kumaliza nguvu ya vyama vya upinzani, kinachofuata ni Taasisi za Dini na baada ya hapo ni kuanza kuumizana wenyewe!
Tweet media one
35
113
820
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Wengine tunawekeza nguvu na hata kuhatarisha maisha yetu kupambania haki na mifumo imara ya utawala kama Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Lakini kinachotutisha ni kasumba ya wanasiasa kufikiri hawawezi kufanikiwa bila kuchafua na kuua wenzao! Hatuwezi kuwa Taifa la washenzi!
32
93
812
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kabla ya Jeshi la Polisi halijatoa taarifa za kiuchunguzi kuhusu wasifu wa 'gaidi' aliyeshambulia na kuua Askari Polisi na raia mmoja jijini Dar es Salaam leo, mitandao ya kijamii imeanza kufichua wasifu wa mtu huyo na Taasisi aliyotoka! Kibo kya Ndesi! Chubha!
47
74
806
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
Ndugu Watanzania! Sisi Askofu Mwamakula tumejulishwa kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amebadilishiwa makosa na kupewa Kesi ya Uhaini usiku huu. Taarifa hii tumepewa na wakili wake, Dickson Matata.
Tweet media one
71
167
829
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Tulikwenda Kibamba kumuona Dkt. Christopher Cyrilo aliyeshikiliwa na Polisi siku 3 akihojiwa kwa kukosoa Serikali mitandaoni. Aliachiwa 29 Septemba kwa dhamana. Anaripoti Police Central mara 3 ndani ya siku 5! Ni sawa na kifungo cha nje! Uhuru wake wa kutafuta ridhiki umefinywa!
Tweet media one
26
87
809
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
Aliyevaa nguo nyeusi pembeni ya Askofu ni Deus aliyeitisha maandamano ya amani katika Mkoa wa Dar, Jumatatu 19 Juni 2023 kupinga Mkataba wa Bandari. Tumeelezwa kuwa anapokea simu za vitisho na ameitwa kwa RPC wa Temeke. Sisi Askofu Mwamakula tunafuatilia kwa karibu taarifa hizo.
Tweet media one
38
130
829
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
4 months
Martin Maranja Masese (MMM) tunaomba rudisha 'ala yako kiunoni'! Ushauri wa Shangazi Fatma Karume ulilenga kutuliza dhoruba na kukuheshimisha. Tunamuomba Mange Kimambi naye asitishe mjadala huu. Sio kawaida yetu, ila mjadala wenu unatutisha. Sauti yetu ni uwakilishi wa wengi
50
71
821
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Wengine wanahamasisha kususia zoezi la Sensa kama Serikali itakataa kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya kabla ya 2025! Serikali nayo inahamasisha kususia mchakato wa Katiba Mpya kabla ya 2025! Huu nao ni mkwamo haijalishi nani ana nguvu! Tusikwamishane, tukae tuzungumze pamoja!
62
78
794
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
13 days
Ukiona watu wanaamua kuvujisha matokeo au hata kujitangaza kabla ya matokeo rasmi hayajatangazwa na Tume ya Uchaguzi, basi ujue ya kuwa watu hao hawaiamini Tume. Ikitokea hivyo, Tume nayo huogopa na huamua kuyatoa matokeo jinsi yalivyo ili kuepuka kusulubishwa
11
124
825
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Mechi ya Simba na Yanga imevurugwa povu kila kona hata Serikali inatetemeka! Uchaguzi Mkuu na wa Serikali za Mitaa vilivugurugwa, kila mtu alichukua hamsini zake! Taifa lililovurugwa watu huhoji yasiyo ya msingi na kuacha ya msingi kwani njia pekee ya wao kuishi ni kuwa wanafiki
46
78
793
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Tumeongea na John Heche! Amesema leo 23 Oktoba, Wagombea Ubunge 64 wa CHADEMA mwaka 2020 walizuiwa kumuona Mwenyekiti wao Mbowe asubuhi pale Magereza ya Ukonga. Heche pia amezuiwa kumuona alipokwenda mchana! Alizuiwa hata kuonana na Mkuu wa Gereza. Hii haikubaliki hata kidogo.
Tweet media one
19
122
777
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
Sisi Askofu Mwamakula tunaelekea nyumbani kwa Balozi Dkt. Slaa muda huu. Tutakuwa pale pamoja na Mheshimiwa James Mbatia na watu wengine. Tutatoa kauli ya pamoja kwa Watanzania wetu mahali pale mchana huu.
26
139
800
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Tumejulishwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa John Pambalu kuwa Katibu Mwenezi wao Twaha Mwaipaya ambaye alikamatwa jana Morogoro, kuwa hadi muda huu hayupo Dodoma wala Morogoro! Hofu imetanda kuhusu wapi alipo. Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kueleza wapi alipo na kumuachia huru
35
144
773
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Mwanamke anakamatwa kwa masuala ya kisiasa, anawekwa ndani kwa zaidi ya siku 6 pasipo kupelekwa Mahakamani! Huu ni ufinyaji haki wa kiwango cha juu anaofanyiwa Neema Mwakipesile wa CHADEMA Temeke! Polisi muachieni Mama huyu akalee watoto wake kama kesho hamtapeleka Mahakamani!
Tweet media one
33
131
758
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 months
Kama Lissu ametukana, vyombo husika vimpeleke mahakamani kujibu jinai. Kama kaisema CCM na Mwenyekiti wake, ni kazi ya Timu ya Propaganda ya CCM kujibu hoja. Ninyi wengine enezeni sera zenu na kama mmekoma kuwa vyama vya siasa, msajili awatoe katika orodha yake mkawe makada kule.
50
142
793
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, Kathrin Steinbrenner alifika Mahakamani kusikiliza Kesi ya Mbowe na wenzake. Alimtia moyo Mbowe kwa Lugha ya Kiingereza akisema: "Never! Never! Never give up"! ("Kamwe! Kamwe"! Kamwe usikate tamaa")! Mbowe alijibu: "Kamwe siwezi kukata tamaa"!
33
159
755
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Tumesikia Rais Samia ameunda Tume ya kupokea maoni ya kurekebisha Jeshi la Polisi na taasisi nyingine za kutoa haki. Kwa maoni yetu, hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali. Badala yake nguvu kubwa ingeelekezwa kuandika katiba mpya kuliko kuendelea kushona viraka kwa gharama kubwa!
Tweet media one
44
117
761
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Tumepata taarifa usiku huu kuwa Mdude ameachiwa bila masharti ye yote! Sauti zetu ndio nguvu yetu. Hakuna jeshi lililowahi kupambana na sauti na kelele za watu likashinda!
Tweet media one
20
86
760
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Hivi hawa watu mnataka waende msituni? Mikutano ya Hadhara mmezuia! Mikutano ya Ndani hamtaki wafanye! Wakikutana kwenye mapagala, mnawakamata! Wakienda Kanisani, mnawakamata na kuwapeleka Mahakamani! Hata vitani inaachwa njia ya adui kuweza kukimbia! Ole wenu! (Ezekieli 33:1-20)
Tweet media one
42
106
736
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Nampongeza Askofu Dkt. Fredrick Shoo kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). Kuchaguliwa kwake ni dalili nzuri kwa CCT katika kuimarisha misingi na madhumuni ya kuanzishwa kwake. Natambua umuhimu wa yeye kuiongoza CCT katika mazingira ya sasa!
Tweet media one
22
64
727
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Kama Wamasai hawako tayari kwenda huko mnakowapeleka hata mkitumia makarandinga haitasaidia. Hakuna binadamu anayelazimishwa kuishi mahali asipopenda, labda mfungwa tu lakini sio mtu huru. Wamasai ni watu huru katika nchi na ardhi yao. Mpeni Waziri Mkuu ujumbe kutoka kwa Askofu!
60
112
714
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Kukamatwa kwa Twaha Mwaipaya kunatokana na ukweli kuwa maandishi yake mitandaoni na harakati zake nchini ni tishio kwa uhai na uhalali wa maslahi ya watawala yasiyo maslahi mapana ya umma. Sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa Serikali ya Rais Samia kumuachia huru bila masharti.
28
103
717
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
We, Bishop Mwamakula would like to inform the general public that we have accepted an invitation to attend and grace the General Conference of the National Council of the main opposition party in Tanzania, CHADEMA on 11 May 2022 in Dar es Salaam.
13
50
722
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Baada ya SSH kusifiwa kwa mageuzi makubwa ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi; mawimbi ya ujambazi na utekaji yanaibuka tena huku baadhi ya watu mitandaoni wakichombeza kuwa ni bora Awamu ya Tano. Huenda nyuma ya mawimbi haya kuna kusudio la kuihujumu na kuifitini Serikali ya Samia!
40
72
697
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Catherine Ruge, the Secretary General for BAWACHA, the Women wing of the opposition party CHADEMA has been arrested today at Kisutu Court in Dar es Salaam. She was attending the hearing of the case of their Chairman, Freeman Mbowe. We call for her release with immediate effect!
Tweet media one
11
130
694
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kuna Mbunge anateseka kutokea Dodoma! Anataka watu wazuiwe kuhoji ila hana shida na wanaosifu! Hajui kuwa kuzuia watu kutoa maoni yao ndio udikiteta na ufashisti wenyewe! Haelewi kuwa kuzuia watu kutoa hisia zao ndio kutaondoa amani na utulivu nchini! Mpelekeeni salaam za Askofu!
32
66
694
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 months
Bunge lilipokuwa la mseto, Spika alikuwa akipambana na Wabunge wa Chama Kikuu cha Upinzani. Baada ya Bunge kuwa la Chama kimoja (CCM), Spika anapambana na Wabunge wa upinzani kutoka ndani ya CCM. Hakuna binadamu aliyewahi kufuta upinzani duniani! Tunasubiria yatakayomkuta Mpina!
25
95
705
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
With Robert Kyagulanyi (Bobi Wine), President of NUP, the main opposition party in Uganda. He was presidential candidate for the general elections of 2021. He was in Dar for the conference of the National Council of the main opposition party in Tanzania, CHADEMA on 11 May 2022.
Tweet media one
7
41
675
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
13 days
It's over! Imetimia!
24
68
709
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Rais Samia amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai! Meza ya Askofu Mwamakula ina kikombe kilichojaa machozi ya watu dhidi ya Sabaya. Uchunguzi dhidi yake utawatendea wengine haki na yeye mwenyewe! Hatua hiyo ya Rais itume ujumbe kwa wababe wengine waliobakia ambao wako wengi pia
30
68
666
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Inaonekana Spika Ndugai alisoma kitabu cha Animal Farm! Bunge chini ya uongozi wake halikumpa Tundu Lissu nafasi ya kusikilizwa na kujitetea, lakini alihoji akiwa katika Bunge hilo hilo chini ya uongozi wake kama kumi na kenda wa CHADEMA walipewa muda wa kusikilizwa na kujitetea!
29
80
674
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kesi ya wana CHADEMA 23 imeendeshwa mwaka mzima bila upande wa Mashtaka kupeleka ushahidi mahususi Mahakamani! Hakimu Mkazi Kisutu amevaa ujasiri, kaipiga kalamu, kaona kuwa hoja za upande wa Mashtaka hazina mashiko! Nguvu za kushinikiza kesi kama hizo imekwenda na Kimbunga Jopo!
22
52
665
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
20 days
Nimemsikiliza Tundu Lissu. Anasema CHADEMA ijibu tuhuma za Mch. Msigwa kinyaraka. Watu waliokomaa kitaaluma huheshimu nyaraka! Ibilisi alimuandama Yesu kinyaraka, akajibiwa kinyaraka (Mathayo 4:1-10). Ukituhumu watu kwa mambo ya nyaraka, na wewe uwe na nyaraka za kuthibitisha!
17
116
695
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Jeshi la Polisi linahitaji kupitiwa na kinyozi! Kitendo cha Kamanda wa Polisi Dodoma kutoa vitisho hadharani mbele ya kamera akiwa na sakari wenye silaha kwa wanawake wanaotaka kwenda Bungeni bila salaha ni fedheha kwa Taifa. Hayo ndiyo mambo yatakayomtesa SSH kama atayanyamazia!
26
68
661
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Mtu ambaye umemnyima haki yake hawezi kukupenda, hawezi kutulia na wala hawezi kuwa na amani na wewe. Endapo mtu huyo ataonyesha kukupenda, kutulia na kuwa na amani na wewe, basi atakuwa anakufanyia unafiki lakini kwa siri akiandaa hujuma dhidi yako na akipata mwanya atakumaliza!
28
113
661
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Tuhuma zilizotolewa na Kigogo katika mitandao ya Twita na Facebook kwa CRDB Bank Plc Millenium Tower kuhusu accounts za staff 17 wanaosemekana kufukuzwa kazi na Clouds Media Live ni nzito, hazitakiwi kupuuzwa! Ipelekwe kurunzi au tochi ili kubaini kama kweli kuna jambo kama hilo!
10
44
670
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Ukipigania ili nduguyo apate cheo katika taasisi uliyopo - Kanisani, Chama cha Siasa au Serikali; jua kuwa unapigania tumbo lako na la nduguyo, huangalii maslahi ya Kanisa, Chama, jamii au nchi!
13
58
642
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
14 days
Hii minong'ono kuwa mawakili wa Zanzibar wanaletwa Dodoma ili kupiga kura Uchaguzi TLS ina ukweli? Kwani mawakili wa Zanzibar ni memba wa Tanganyika Law Society (TLS)? Kama sio memba basi wasiruhusiwe kuingia ukumbini kwani si wanajulikana?
24
82
678
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Rais Samia Suluhu, mtangulizi wako Magufuli alivunja Katiba alipotoa tamko la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini ambalo bado linaitesa nchi kwa kuwa Polisi na Watendaji wanendelea kulitekeleza. Tunakusihi utoe tamko la ama kutengua au kuunga mkono ili tuujue msimamo wako!
23
75
645
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 months
Kinana alinukuliwa akisema: "Hakuna Tume ya Uchaguzi duniani ambayo Rais hana mamlaka nayo". Je, kauli hiyo ina ukweli gani kwa Tume za Uchaguzi za Malawi, Afrika Kusini, Zambia, Nigeria, Ghana na Kenya? Kama Rais ana mamlaka na Tume Huru ya Uchaguzi, uhuru wa Tume sasa ni upi?
Tweet media one
98
131
669
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Viongozi wanaong'ang'ania madaraka badala ya kuwajibika na kujiuzuru wanapogundua kuwa wameharibu mambo, hujiandalia fedheha kubwa mbele. Lakini wale wanaowajibika na kujiuzuru mara hujijengea heshima kubwa wao wenyewe na huzijengea heshima taasisi zao pia! Kujiuzuru sio udhaifu!
Tweet media one
16
80
615
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
Chatu hawezi kumeza mtu au mnyama kama kuna keleleza watu. Atakachofanya ni kuachia au hata kutapika windo lake ili ajinasue asije akauawa. Ndicho kinachotokea kwa Dkt. Slaa, Mwabukusi na Mdude. Wanapikwa wazima
14
132
626
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Rais Samia ameahidi kukutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini ili kujadili kuhusu Demokrasia. Hili ni jambo lililotutia moyo kama Viongozi wa Dini na tunaliunga mkono. Sisi tunaendelea na jitihada zetu za kuhamasisha umma kuhusu kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.
17
68
610
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Magazeti, Televisheni na Radio nchini Tanzania vinashtumiwa na Wamasai kuwa vimekacha kuandika habari juu ya vurugu za Loliondo na Ngorongoro kwa kuogopa mamlaka. Kazi hiyo inafanywa kwa uaminifu na watu binafsi mitandaoni. Hii ni aibu kubwa sana kwa media.
45
89
614
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
1 year
Mwanzoni walimwandikia Mwabukusi kumtaka afike Kituo cha Polisi Mbeya. Alitii, wakamuweka ndani kisha wakamuachia. Leo wamemvizia kama mwizi. Hawajasema yeye na Mdude wako Kituo gani cha Polisi hadi sasa. I am smelling something fishy! Wasiugue magonjwa ya ajabu ndani ya miezi 8.
22
136
620
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kama hakuna Sheria, tusilazimishe wala tusishawishi watu kupokea chanjo ya Covid 19; na pia tusilazimishe wala tusishawishi watu kukataa chanjo ya Covid 19. Kufanya mojawapo kati ya hilo ni UUAJI wa makusudi! Badala yake tutoe elimu kuhusu faida na hasara ya chanjo ya Covid 19.
Tweet media one
24
65
602
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Sisi Askofu tungekuwa karibu na Loliondo na Ngorongoro tungevaa majoho ya Kiaskofu na kuwa katikati ya umati wa Wamasai wanaodai haki zao lakini wanamiminiwa risasi za moto. Viongozi waliotoa amri ya kuumiza watu kule Umasaini na waliotekeleza amri hiyo, Mungu atawafedhehesha!
56
109
601
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
9 months
Tumeongea na wakili Boniface Mwabukusi muda huu. Baada ya mawakili wake 9 kujitoa jana, ilibidi ajitetee mwenyewe. Maaumuzi yatatolewa Januari 2023. Lakini pia tumesikia kauli ya Rais wa TLS jioni hii. Hicho ndicho tulichotaka kuwa TLS itoke kutoka mafichoni.
Tweet media one
14
84
613
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
CDF Generali Mabeyo! Vijana 854 waliopata mafunzo ya kijeshi na kukaa kambini muda wote huo kufukuzwa ghafla na kurudishwa uraiani ni hatari kwa usalama wa raia. Tumshauri Rais warudishwe, ikiwezekana wasambazwe katika majeshi mbalimbali. Ilikuwa ni haki yao kikatiba kudai haki!
82
35
591
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Rais anamsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kilimanjaro yote inasherekea! Ni kama wametolewa kutoka katika kongwa la utumwa! Hapa kuna somo zito. Rais aangalie Mikoa na Wilaya nyingine ambako kuna watawala aina ya Sabaya! Akawaondoe ili kurudisha imani ya wananchi kwa viongozi
26
49
582
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Inatia moyo kuona sauti za watu mashuhuri za kutaka Mbowe aachiliwe bila masharti zisikiongezeka! Lakini itakuwa na nguvu zaidi endapo watu hao watachukua hatua pia za kufika Mahakamani angalau hata mara moja. Mabalozi wa nchi za nje wanaonekana kuwa na mzigo zaidi kuliko sisi!
7
78
602
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
"Na kondoo wengine ninao ambao sio wa kundi hili. Nao imenipasa kuwaleta. Nao wataisikia sauti yangu na kutakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja" - Yesu Kristo (c.33 BK). Pia unaweza kuyasoma haya katika Yohana 10:16. Nini kimekushangaza? Nini maoni yako?
Tweet media one
19
63
606
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Nimeona BAWACHA wakimwimbia wimbo Ndugai! Mfalme Sauli alielewa fika maana ya nyimbo za wanawake! Kwamba, zilibeba unabii dhidi yake. Wanawake wakikusifu una heri kama walivyomsifu Daudi, lakini wakikuimbia nyimbo za manung'uniko, unapaswa kujitathimini! Ogopa machozi ya wanawake
20
78
580
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Kuna Wachungaji walimpelekea baba yangu kijijini maneno ya uwongo kuhusu mimi. Alipomaliza kuwasikiliza akanipigia simu, akaongeza sauti kisha akaniambia niongee nao. Akawageukia wao na kuwaambia wanieleze mimi kile walichomueleza yeye. Walitamani ardhi ipasuke!
28
54
596
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Unaacha kumkamata Askofu aliyewakaribisha, badala yake unawakamata waliokaribishwa! Hii ni hekima ngeni ambayo haijawahi kujaribiwa hata katika zama zilizotangulia zamani zetu! Tutatoa kauli endapo hao waliokamatwa hawataachiwa huru!
Tweet media one
24
103
580
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Askofu mmoja ananiambia kuwa Zanzibar bei ya lita moja ya mafuta ya Petroli ni Sh. 2600 wakati huku Tanganyika bei ya lita moja ni Sh. 3900. Nimemjibu kuwa asichanganye dini na siasa! Sasa anaanza kunishangaa tena! Muda ni hakimu mzuri, tutaelewana tu!
60
59
577
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Natamani Mashehe wa Uamsho waachiwe. Kuwa Mahabusu miaka 8 ni kufinya haki zao. Ushauri wa Askofu Mwamakula kwa waumini wao ni kuwa, kama kila muumini angelipaza sauti katika ukurasa wake, Mashehe wangelishaachiwa, kelele zingelikuwa kubwa. Serikali ina uwezo wa kufuta tuhuma zao
26
80
562
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
2 years
Sisi Askofu tumetoa tamko la kukemea vurugu zinazolenga kukivuruga chama cha NCCR Mageuzi na kuwakemea watu, makundi na taasisi zilizo nyuma ya vurugu hizo ndani ya chama hicho. Tumetoa wito kwa watu kuheshimu taratibu na Katiba ya NCCR Mageuzi. Kuvuruga upinzani ni uhalifu zaidi
18
82
570
@EmmausAskofu
Askofu Emmaus B Mwamakula
3 years
Hawa Maaskofu na Mashehe! Waumini wao ambao ndio watoaji sadaka na kujenga nyumba za ibada ndio waliojaa mahabusu kutokana na matukio ya uonevu ya Uchaguzi wa Oktoba 2020. Wakiitwa kwenye mikutano ya Serikali hufanya sala ndefu sana pasipo hata kuwasemea na kuwatetea waumini wao
28
70
552